1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 50 wauawa na ADF Congo Mashariki

30 Mei 2022

Watu wapatao 51 wameuawa na wengine kadhaa wametekwa nyara wakati wa shambulio la waasi wanaodaiwa kutoka kundi la ADF katika wilaya ya Beni na Ruenzori katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4C3MY
Kongo Brazzaville | Kongolesische Soldaten
Picha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Mauwaji ya watu 37 yaliyofanywa na wapiganaji wa ADF yalifanyika katika kijiji cha Beu Manyama katika wilaya ya Beni, mwishoni mwa juma lililopita, na watu 14 waliuawa katika mji mdogo wa Bulongo, kilomita thelathini mashariki ya Beni na malori saba yalichomwa moto, usiku wakuamkia Jumatatu. 

"Tuliaokota hadi miili 27 siku ya Jumamosi na tumeokota mingine 10," alisema Kinos Katuho, rais wa shirika la kiraia la eneo hilo wakati akizungumza na shirika la habari la Ujeruani, dpa, Jumapili jioni.

Soma pia: Waasi wa ADF wafanya mauaji huko Ituri DRC

Alisema wahanga waliuawa katika majumba yao, katika kijiji cha Beu-Manyama, kwa kutumia mapanga na risasi za moto, na wapiganaji kutoka kundi la waasi la Allied Democratic Froces, ADF.

DR Kongo | Soldaten in einer Militäroperation gegen bewaffnete Kräfte
Wanajeshi wakifanya doria ya pamoja dhidi ya makundi ya waasi katika wilaya ya Beni, Mashariki mwa DRC.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Congo katika eneo la Beni, Kapteni Anthony Mwalushay, alithibitisha haya na kusema jeshi liliuwa wapiganaji saba wa ADF katika kujibu shambulizi hilo.

Mauaji mengine yalitokea katika kijiji cha Bulongo kilichoko umbali wa kilomita 40 mashariki mwa Beni, katika wilaya ya Ruenzori, ambako kulingana na shirika la haki za binadamu na afisa wa serikali ya mtaa, raia 15 waliuawa.

Soma pia: Raia zaidi ya mia moja wauliwa Kongo mnamo wiki moja

Wapiganaji wanaoaminika kutoka ADF walivamia kijiji hicho cha Bulongo katika mkoa wa Kivu Kaskazini baada ya giza kuingia Jumapili, na kuharibi majumba na kuua wakaazi waliokutana nao njiani, meya wa manispaa Jean Paul Katembo aliliambia shirika la habari la Reuters.

Washambuliaji waliuwa watu 15 na kuchoma moto wagari sita, alisema rais wa shirika la kiraia la sekta ya Ruenzori Ricardo Rupande.

"Ilikuwa majira ya saa tatu usiku niliposikia milio mikubwa. Hatua ya kwanza ilikuwa kukimbia kwa sababu nilidhani walikuwa ADF. Waliuwa kaka zetu na dada zetu 15," alisema mkaazi wa Bulango Meza Milan.

Soma pia: Vikosi vya Uganda vyaingia Congo vikiwasaka waasi

Kundi la ADF linajitanabahisha kama tawi la kundi la Dola la Kiislamu katika eneo la Afrika ya Kati. Wametuhumiwa kwa mashambulizi kadhaa mashariki mwa Congo na Uganda.

Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Waasi wa ADF wameuawa watu na kuchoma majumba yao.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Majeshi ya Congo na Uganda yalianzisha operesheni ya pamoja dhidi ya ADF mnamo mwezi Novemba, lakini yameshindwa mpaka sasa kudhibiti vurugu za kundi hilo.

Kwa mujibu wa Marekani, takribani makundi 130 ya silaha yako mashughuli mashariki mwa Congo, mengi yao yakijihusisha na udhibiti wa maliasili za thamani.

Ikiwa na takribani wakaazi milioni 90, DRC ina utajiri mkubwa wa maliasili kama vile shaba, cobalt, dhahabu na almasi.