1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa ADF wafanya mauaji huko Ituri DRC

Admin.WagnerD12 Aprili 2022

Waasi wa ADF huko Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo hapo jana wamefanya mauaji ya watu zaidi 30 katika vijiji vya Machwalo, Shaurimoya na Mangusu wilayani Irumu katika mkoa wa Ituri.

https://p.dw.com/p/49pch
Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

 Mauwaji hayo yanatokea wakati majeshi ya Congo pamoja na Ugandayanakabiliana na waasi wa ADF katika eneola mashariki ya Beni pamoja na Irumu. 

 Christophe Munyanderu, mratibu wa shirika la kutetea haki za binaadamu CRDH katika wilaya ya Irumu, alitangaza  idadi ya watu waliouawa na ADF wilayani humo.

Soma zaidi:M23 yatangaza kujiondoa vijiji ilivyoviteka Congo

Alisema awamu ya kwanza waligundua watu wasiopungua 20 kadhalika uharibifu mkubwa wa mali katika maeneo hayo ya vijiji.

Manusura wa mashambulizi hayo yaliotokea  jana, waliiomba serikali  kuingilia kati ili kunusu maisha ya raia wasio na hatia.

"tunaiomba serikali iingilie kati mauaji haya"  mmoja wa manusura alimwambia mwandishi wa DW katika eneo hilo na kuongeza kuwa "nyumba na magari yameharibika"

Watetezi wa haki za binadamu waingilia kati

Mauwaji wanayoyafanya na waasi wa ADF katika wilaya za Beni na Irumu, yamewasikitisha wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini DRC.

Christophe Munyanderu, mratibu wa moja wapo ya mashirika hayo CRDH, anatoa mwito huu kwa gavana wa jeshi Luteni Jenerali Luboya Nkashama Johnny

Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
nyumba zilizoharibiwa na mashambulizi ya waasiPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Soma zaidi:Raia 13,000 waingia Uganda wakikimbia mapigano ya M23

Alimtaka Gavana anapokuja kupambana na waasi hao akamilishe ahadi yake ya kumaliza mauaji haya."anapokuja kupigana na adui ahakikishe anamaliza ubaya wote katika eneo hili" Alisisitiza.

Jeshi la DRC lasisitiza kuendelea na oparesheni za kijeshi

Msemaji wa jeshi la Congokatika mkoa wa Ituri luteni Jules Ngongo, kufuatia mauaji hayo alitangaza kuendelea kwa operesheni za kijshi zenye dhima ya kuyaondoa makundi ya waasi katika maeneo hayo.

Aliwataka wakaazi wa eneo hilo kuwasalia majumbani kwa utulivu wakati jeshi likiendeleza mapambao yake ya kumaliza vikundi hivyo vinavyotekeleza mauaji kwa raia na uporaji wa mali.

Symbolbild | DR Kongo | Anschlag der Alliierte Demokratische Kräfte Kongo
Wanajeshi wa DRC wakiwa katika oparesheni ya kijeshiPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Aliongeza kuwa waasi hao wa ADF ambao wamekuwa wakiendeleza vitendo vya uporaji na mauaji kwa raia wasio na hatia,wameishiwa nguvu kutokana na mapambano makali na jeshi la nchi hiyo.

soma zaidi:Watu 30 wauawa katika mashambulizi ya waasi Kongo

"ADF wameishiwa nguvu na ndio katika kutoroka kwao walifanikiwa kuwauwa wakaazi na mauwaji hayo yanatuhuzunisha" Ngongo alinukuliwa na vyombo vya habari.

waasi wawaachia huru wajumbe wa amani

Wajumbe wa amani wa Rais Félix Antoine Tshisekedi katika mpango wa kuwahamasisha raia wa Ituri kulinda amani, waliokuwa wanashikiliwa na wapiganaji wa CODECO, wameachiwa huru na tayari wamewasili mjini Bunia.

Duru karibu na Kikosi kazi hicho zimesema kuwa, wajumbe hao akiwemo kiongozi wao Thomas Lubanga, walifanikiwa kutoroka kutoka mikononi ya CODECO.

Ripoti hiyo hata hivyo haijathibitishwa wala kukanushwa na duru karibu na CODECO.