1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Marekani yauwa wapiganaji 12 wa Al-Shabaab Somalia

13 Februari 2023

Marekani imesema shambulio la ndege katika eneo la mbali nchini Somalia limeuwa wanachama 12 wa kundi la wapiganaji la Al-Shabaab.

https://p.dw.com/p/4NOp6
Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM, imesema uvamizi huo wa angani ulifanyika siku ya Ijumaa, umbali wa karibu kilomita 500 kutoka mji mkuu Mogadishu. Lilikuwa shambulio la nne la Marekani dhidi ya  al-Shabab  mwaka huu, na limefikisha jumla ya vifo 48 kwa kundi hilo.

Serikali ya Somalia imetaja idadi ya vifo kutokana na shambulio la Ijumaa kuwa 20, ikiwa ni kubwa zaidi kuliko iliyodaiwa na Washington. Kundi la  Al-Shabab  ambalo linataka kuweka utawala unaofuata tafsiri kali ya Uislamu, limekuwa likipambana na serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2006.

Kundi hilo limefurushwa nje ya  Mogadishu  na maeneo mengine, lakini linaendelea kushambulia maeneo ya kijeshi na kiraia.