1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Al Shabaab yawaua wanajeshi 7 wa Somalia

Saumu Mwasimba
20 Januari 2023

Wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Alshabab leo wameshambulia na kuua kiasi wanajeshi 7 katika kambi ya wanajeshi wa Somalia katika mji uliokombolewa na serikali.

https://p.dw.com/p/4MUpU
Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Taarifa ya mashambulizi dhidi ya wanajeshi hao imetolewa na wizara ya habari na kundi hilo la wanamgambo. Afisa mmoja kwenye kambi hiyo ya kijeshi iliyoko kwenye mji wa katikati ya Somalia wa Galcad ameliambia shirika la habari la Reuters, shambulio hilo hatiame lilidhibitiwa.Miongoni mwa waliouwawa ni naibu kamanda wa kambi hiyo ya jeshi aliyekuwa sehemu ya wanajeshi waliopewa mafunzo na Marekani. Shambulio hilo linaonesha kitisho kinachosababishwa na Alshabab kwa wanajeshi wa Somalia, licha ya operesheni iliyoanzishwa na serikali mwaka jana kuonesha ufanisi dhidi ya wanamgambo hao.