1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia karibu Kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki

Veronica Natalis
24 Novemba 2023

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo wameikaribisha rasmi Somalia kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo inayofikisha sasa idadi ya nchi nane wanachama.

https://p.dw.com/p/4ZPy1
Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Picha: Abukar Mohamed Muhudin/AA/picture alliance

 Hayo yametangazwa katika mkutano wa kilele wa kila mwaka wa  wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika leo mjini Arusha Tanzania.

Mwenyekiti wa wakuu wa nchi wanachama aliyemaliza muda wake na Rais wa Burundi , alitangaza rasmi azimio la kikao cha wakuuwa nchi kuhusu maombi ya Somalia kujiunga na jumuiya hiyo kuwa yamekubaliwa.

"Tumekubali  maombi ya jamhuri ya shirikisho la nchi  ya Somalia kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki, hatua zingine zote za kisheria zinazofuata."

Alitangaza katika mkutano huo mwenyekiti anaemaliza muda wake Ndayishimiye.

Aliongeza kuwa baada ya tangazo hilo taratibui zaidi za kisheria zinazofuata zitasimamiwa na mwenyekiti ajae  wa wakuu wa nchi za jumuiya hyo.

Soma pia:Wakuu wa nchi za EAC wajadili mabadiliko ya tabia nchi

Somalia inayopakana na nchi ya Kenya upande wa kusini magharibi, inaweka idadi ya jumla ya nchi nane ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo kongwe barani Afrika.

Kuhusu ripoti ya maendeleo ya mazungumzo ya Nairobi kuhusu suala la usalama mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Ndayishimiye amesema kwamba wakuu wa nchi wameelekeza majeshi ya jumuiyaya Afrika Mashariki EAC pamoja jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC wakutane na kuandaa mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia suala hilo.

Alisema imeelekezwa kwamba majeshi ya Afrika Mashariki na SADC wakutane ili waandae mapendekezo na kuyawasilisha kwa mawaziri wa ulinzi na usalama, wa nchi wanachama.

"Mapendekezo hayo yatahusu namna ya kulishughulikia suala la amani mashariki mwa Kongo.” 

Mzozo wa Kongo wachukua mjadala mpana

Kongo inayojiandaa na uchaguzi mkuu wa Rais unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu, imekuwa ikikabiliwa na mzozo wa kiusalama eneo la mashariki huku hata hivyo jumuiya ya Afrika Mashariki ikitupiwa lawama ya kutokuwa na mikakati thabiti ya kulimaliza suala hilo.

Kikosi cha EAC chatakiwa kuondoka Congo

Marais karibu wote waliozungumza katika mkutano huo wameonesha nia yao ya dhati ya kushirikiana na Kongo kumaliza mzozo huo kwa kuhakikisha wanakubaliana na mbinu za kitaalamu kwa matokeo chanya.

Soma pia:Congo yataka vikosi vya Afrika Mashariki viondoke DRC

Rais wa Kenya Willium Ruto ameuwambia mkutano huo wa kilele kwamba kama wanajumuiya ya Afrika Mashariki kamwe hawataitelekeza kongo.

"Tutakubaliana na kufuata mbinu zote kwa kushirikiana na wenzetu wa SADC na kuona ni jinsi gani suala hilo litashughulikiwa."

Rais Ruto aliongeza kwambajitihada hizo zinafanyika ni kwa usalama kwa maslahi mapana ya raia wa Kongo na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Katika mkutano huo pia, Rais wa Sudan Kusin Salva Kiir amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa wakuuwa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Nafasi hiyo huwa ni ya mzunguko kwa nchi zote wanachama na hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.