1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Julian Nagelsmann anayo nafasi ya kuinoa Ujerumani?

21 Septemba 2023

Ni asilimia 33 tu ya Wajerumani ndio ambao wangependelea kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4WebO
Julian Nagelsmann wird neuer Bundestrainer
Kocha wa zamani wa Bayern Munich Julian NagelsmannPicha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/picture alliance

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na  taasisi ya YouGov, ni asilimia 33 tu ya Wajerumani ndio ambao wangependelea kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani.

Wengine 18% wanapinga Nagelsmann kuwa mrithi wa Hansi Flick, wakati 24% hawamfahamu kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich. 

Soma zaidi:  Ujerumani yamfuta kocha wa timu ya taifa, Hansi Flick kutokana na rekodi mbovu ya hivi karibuni

Utafiti huo ulifanywa tarehe 20 Septemba kwa watu 2,277 walio na umri wa zaidi ya 18.

Bundestrainer Hans-Dieter Flick
Hans Flick, Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ambaye ametimuliwa kufuatia matokeo mabaya.Picha: Sven Simon/imago images

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, Nagelsmann tayari amefikia makubaliano na Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) kuchukuwa kazi hiyo, huku Rais wa DFB, Bernd Neuendorf, akisema wako kwenye "mazungumzo mazuri."

Ujerumani inahitaji kocha mpya baada ya Flick kutimuliwa Septemba 10 kwa kushinda mara nne tu katika michezo yake 17 iliyopita, iliyojumuisha mechi ya pili mfululizo ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia na vipigo vinne katika michezo mitano iliyopita bila ushindi.