1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ujerumani aonya juu ya ugaidi kanda ya Sahel

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Svenja Schulze ameonya kuwa ugaidi na malengo ya Urusi, yanatishia amani ya kanda ya Sahel katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara.

https://p.dw.com/p/4dBWH
Ujerumani Berlin | PK BMZ na Unicef ​​​​| Svenja Schulze
Svenja Schulze, Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, Berlin, Februari 23, 2024.Picha: Ute Grabowsky/photothek/IMAGO

Shulze ametoa kauli hiyo wakati akianza ziara nchini Burkina Faso na Benin kwa mazungumzo ya kisiasa jana Jumatatu. Schulze amekuwa waziri wa kwanza barani Ulaya kuiziuru Burkina Faso tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi mwezi Septemba mwaka 2022, yaliyomweka madarakani Ibrahim Traoré kuwa kiongozi wa taifa hilo. WaziriSchulze ni mwenyekiti wa muungano wa Sahel ulioundwa na Ujerumani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya ili kuyasaidia mataifa ya ukanda huo wa Sahel. Ujerumani pia ndio mfadhili wa nne mkubwa wa muungano huo. Burkina Faso taifa lenye wakaazi takribani milioni 23, limekuwa chini ya mashambulizi ya makundi  ya kigaidi kwa miaka kadhaa.