1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 5 wafariki kwenye kiwanda cha roketi na nchini Uturuki

Tatu Karema
10 Juni 2023

Mlipuko kwenye kiwanda cha kutengeneza roketi na vilipuzi nchini Uturuki umesababisha kuporomoka kwa jengo moja na kuwauwa wafanyakazi watano waliokuwa katika jengo hilo

https://p.dw.com/p/4SQ2K
Feuer in Israel
Picha: AP

Sahin, amewaambia wanahabari kwamba mlipuko huo ulitokea katika saa za asubuhi kwenye kiwanja cha shirika la sekta ya mitambo na kemikali linalomilikiwa na serikali viungani mwa mji mkuu Ankara. Shirika la habari la kibinafsi NTV limeripoti kuwa moshi wa kijivu ulionekana ukipaa kutoka kiwanja hicho huku ambulansi na malori ya kuzima moto yakifika katika eneo hilo.

Huenda mlipuko ulisababishwa na mmenyuko wa kemikali

Jamaa za familia pia walifika katika eneo hilo kuwajulia wapendwa wao. Sahin ameongeza kusema kwamba mlipuko huo huenda ulisababishwa na mmenyuko wa kemikali wakati wa kutengeneza baruti na kwamba waendesha mashtaka wameanzisha uchunguzi rasmi wa tukio hilo.