1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroEthiopia

Watu 400 wafa njaa mikoa ya Tigray na Amhara

Lilian Mtono
31 Januari 2024

Takribani watu 400 wamekufa kwa njaa katika mikoa ya Tigray na Amhara nchini Ethiopia katika miezi ya hivi karibuni. Takwimu hizo zimetolewa na taasisi ya taifa inayofuatilia utawala bora.

https://p.dw.com/p/4bsrX
Wakaazi katika jimbo la Tigray
Wakaazi katika jimbo la Tigray Picha: Million Hailesilassie/DW

Maafisa katika mikoa ya Tigray na Amhara walikuwa wameripoti vifo vilivyotokana na njaa katika wilaya za mikoa hiyo, lakini serikali ya shirikisho ya Ethiopia ilisisitiza ripoti hizo si za kweli.

Taasisi hiyo iliwatuma wataalamu katika mikoa hiyo iliyokumbwa na ukame na vita vilivyomalizika miezi 14 iliyopita na kugundua kwamba jumla ya watu 351 walikufa kwa njaa katika mkoa wa Tigray ndani ya kipindi cha miezi sita iliyopita na vifo vya watu wengine 44 katika mkoa wa Amhara.

Kwa mujibu wa asasi ya utoaji wa misaada ya chakula katika mkoa wa Tigray ya Food Cluster, ni asilimia 14 tu ya watu milioni 3.2 waliolengwa kupatiwa msaada wa chakula na wa kibinadamu na mashirika ya Tigray, walipokea chakula kufikia Januari 21.