1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati na raia wa Hong Kong waandamana nchini Taiwan.

Zainab Aziz
10 Juni 2023

Mamia ya wanaharakati, wanafunzi, na raia wa Hong Kong wanaoishi Taiwan wameandamana katika barabara za jijini Taipei kuhimiza watu kuendelea kuunga mkono demokrasia na haki za binadamu huko Hong Kong.

https://p.dw.com/p/4SQHe
Taiwan Taipei | Protest gegen Sicherheitsgesetz in Hong Kong und Inhaftierung von politischen Gefangenen
Picha: Wiktor Dabkowski/picture alliance

Hafla hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa pamoja wa mashirika ya kitaifa na kimataifa yasiokuwa ya serikali ikiwa ni pamoja na kundi la raia wa Hong Kong wanaoishi Taiwan na shirika la Amnesty International kuadhimisha mwaka wa nne wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia yaliohusisha mamilioni ya wakazi wa Hong Kong.

Licha ya mvua kubwa, washiriki wengine wakiwa wamevalia fulana nyeusi kama waandamanaji wa Hong Kong wa mwaka 2019, waliandamana katika eneo la kati la Taipei. Inakadiriwa kwamba watu elfu moja walishiriki katika maandamano hayo.

Washirika hao walisema kuwa hawapaswi kusahau maandamano yaliopita ya demokrasia mjini Hong Kong ama wanaharakati ambao kwasasa wamefungwa katika eneo hilo.