1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Wahouthi wazilenga meli za Marekani, Washington yajibu

6 Machi 2024

Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wamesema wamefanya operesheni ya kijeshi iliyozilenga kwa makombora na droni meli mbili za kivita za Marekani kwenye Bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4dCt8
Wahouthi | Sanaa| Yemen
Waasi wa Houthi wamekuwa wakitumia makombora ya masafa kuzilenga meli kwenye njia ya Bahari ya Shamu.Picha: Mohammed Mohammed/Xinhua News Agency via picture alliance

Taarifa hiyio imetolewa na msemaji wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, Yahya Sarea kupitia hotuba kwa njia ya televisheni.

Hata hivyo kamandi ya jeshi la Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, centcom, imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuyadungua makombora kadhaa yaliyozilenga meli zake yaliyofyetuliwa kutokea maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi.

Kwenye taarifa yake, centcom, imesema makombora matatu na na droni tau zilisambaratishwa kabla ya kufanya uharibifu.

Waasi wa Houthi wamekuwa wakizilenga meli za mizigo kwenye ujia wa kibiashara wa Bahari Nyekundu kwa kile wanachosema ni kushinikiza Israel isitishe mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza.

Marekani na nchi nyingine kadhaa za magharibi zimekuwa zikifanya operesheni za pamoja kuzima hujuma za kundi hilo.