1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen, Sanchez ziarani Mauritania

Bruce Amani
8 Februari 2024

Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wanazuru Mauritania kuzungumzia udhibiti wa wimbi la wahamiaji haramu kwenda Ulaya.

https://p.dw.com/p/4cAhy
Rais Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania.
Rais Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania.Picha: GABRIEL BOUYS/AFP/Getty Images

Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wanazuru Mauritania leo kwa lengo la kuisaidia nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuudhibiti mmiminiko wa uhamiaji haramu kwenda Ulaya wakati wasiwasi ukiendelea kukuwa wa kuongezeka idadi ya wahamiaji.

Von der Leyen na Sanchez wanatarajiwa kuahidi msaada wa euro milioni 200 watakapokutana na Rais Mohamed Ould Ghazouani katika mji mkuu, Nouakchott.

Uhamiaji unatarajiwa kutawala mjadala katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya mwezi Juni wakati kukiwa na ongezeko la vita vya maneno vya kupinga uhamiaji kutoka kwa vyama vya mrengo wa kulia.