1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaonya kusambaratika kwa mpango wa usafirishaji nafaka

7 Aprili 2023

Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amezionya leo hii nchi za Magharibi kuhusu kusambaratika kwa makubaliano ya usafirishaji nafaka za Ukraine, ikiwa vikwazo vya mauzo ya nafaka za Urusi havitaondolewa.

https://p.dw.com/p/4Pp23
Türkei Ankara | Russischer Außenminister Lawrow
Picha: Valeriy Sharifulin/Sputnik/IMAGO

Onyo la Lavrov linajiri baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, kusema mwezi uliopita kwamba Moscow inaweza kusitisha ushiriki wake katika mpango huo ikiwa masharti yake hayatozingatiwa.

Mkataba wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi ulisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki ili kupunguza mzozo wa chakula duniani kufuati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Soma pia: Mpango wa usafirishaji nafaka za Ukraine waongezewa muda

Urusi na Ukraine ni wazalishaji wakuu wa bidhaa za kilimo duniani, ikiwa ni pamoja na ngano, shayiri, mahindi na mafuta ya alizeti. Urusi inaongoza pia kwenye soko la mbolea.