1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaanza mazoezi ya kijeshi katika ukanda wa Arctic

11 Aprili 2023

Vikosi vya Urusi vimeanza mazoezi makubwa kabisa ya kijeshi katika Bahari ya Arctic, kwa mujibu wa kamandi ya jeshi la majini la Urusi upande wa kaskazini.

https://p.dw.com/p/4PuW2
Russland Luftwaffenbasis Engels | Tupolew Tu-160
Picha: Misha Japaridze/AP/picture alliance

Mazoezi hayo yanajumuisha wanajeshi karibu 1,800, manowari zipatozo 15 na ndege za kivita 40. Kulingana na kamandi hiyo, mazoezi hayo yana malengo ya kulinda usalama wa biashara za Urusi zinazopitia baharini pamoja na njia zake za majini, kama ujia wa kaskazini mashariki.

Mazoezi hayo yatahusisha pia majaribio ya mawasiliano  kati ya vikosi vya angani, ardhini na vya majini.

Vikosi vya NATO, pia viliwahi kufanya mazoezi kama hayo katika ukanda wa Arctic, baada ya Urusi kuivamia kikamilifu Ukraine, mwaka uliopita.