1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kujibu baada ya Iceland kufunga ubalozi wake Moscow

Tatu Karema
10 Juni 2023

Urusi imesema leo kuwa ''itajibu'' baada ya Iceland kuwa taifa la kwanza kusimamisha shughuli zake za ubalozi mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4SQME
Russland Sotschi | Wladimir Putin
Picha: HOST PHOTO AGENCY/REUTERS

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema kuwa vitendo vyote vya Iceland

vinavyoipinga Urusi vitasababisha majibu na kuishtumu Iceland kwa kuharibu uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Wizara hiyo imeongeza kuwa itazingatia uamuzi huo usio wa kirafiki watakapoanzisha uhusiano na Iceland katika siku zijazo.

Iceland kufunga ubalozi wake Moscow Agosti mosi

Hapo jana, Iceland imesema kuwa itaahirisha shughuli zake katika ubalozi wake mjini Moscow kuanzia Agosti mosi na kuitaka Urusi kupunguza shughuli zake nchini Iceland. Waziri wa mambo ya nje wa Iceland Thordis Gylfadottir, amesema, hali ya sasa hairuhusu nchi yake kuendelea kutoa huduma katika ubalozi wake nchini Urusi.