1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaelezea taarifa mchanganyiko kuhusu vita Ukraine

Tatu Karema
10 Juni 2023

Serikali ya Uingereza leo imeelezea taarifa mchanganyiko kuhusu mapigano kati ya vikosi vya Ukraine na vya Urusi vinavyopigana katika maeneo ya Kusini na Mashariki mwa Ukraine katika muda wa saa 48.

https://p.dw.com/p/4SQ2J
Ukraine, Bachmut | ukrainische Soldaten nahe der Front
Picha: REUTERS

Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Uingereza, imesema kuwa katika baadhi ya maeneo, vikosi vya Ukraine vimeonekeana kupata ushindi na kupenya safu ya kwanza ya ulinzi wa Urusi huku katika maeneo mengine, ufanisi wa Ukraine ukionekana kuwa wa kasi ya chini.

Hatua za Urusi zimekuwa za mchanganýiko

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa hatua za Urusi zimekuwa za mchanganyiko na kwamba baadhi ya vikosi vyake vinatekeleza operesheni thabiti huku vingine vikijiondoa katika hali isiyoeleweka wakati ripoti zikielezea kuweko kwa majeruhi wa Urusi wanapojiondoa kupitia maeneo yao ya migodi.