1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania na Msumbiji wajadili kupambana na uasi

Lilian Mtono
28 Januari 2022

Viongozi wa Msumbiji na Tanzania wamekutana leo kujadili uasi wa itikadi kali ambao Maputo imeyaita majeshi ya kikanda kusaidia kuukabili.

https://p.dw.com/p/46EYz
Mosambik Pemba | Filipe Nyusi
Picha: DW

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amekutana leo na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mji wa kaskazini mwa Pemba, mji mkuu wa mkoa wa Cabo Delgado ambao wanajeshi wa SADC na Rwanda waliisadia Msumbiji kuuokomboa kutoka kwa wanamgambo wa itikadi kali mwezi Agosti.

Soma Zaidi: Wanajeshi wa nchi za jumuiya ya SADC kupelekwa Msumbiji

Hakuna kati ya hao viongozi aliyefichua maelezo zaidi ya mazungumzo hayo, lakini Nyusi aliashiria kuwa anataka kuendelea kuungwa mkono kutoka kwa mataifa ya kikanda. Rais Samia amesema amekwenda kusisitiza dhamira ya nchi yake kusimama pamoja na Msumbiji kwa ajili ya maendeleo ya masuala ya amani na usalama.

Mapigano kaskazini mwa Msumbuji mara kwa mara yamesambaa na kuingia katika upande wa mpaka wa Tanzania, ambayo ilipeleka wanajeshi wake nchini humo chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC.

Mosambik | Besuch Filipe Nyusi und Paul Kagame in der Provinz Cabo Delgado
Maraida wa Rwanda paul Kagame (kushoto) na Filipe Nyusi wa Msumbiji baada ya kukagua vikosi vilivyokuwepo katika mji wa Pemba katika mkoa wa Cabo Gelgado.Picha: Simon Wohlfahrt/AFP/Getty Images

Nyusi amesema Tanzania mara zote imesimama nao na kuwa tayari kutoa msaada kwa Msumbiji chini ya ujumbe wa kulinda amani wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, SAMIM. "Kwenye mazungumzo yetu tumeangazia namna ushirikiano wetu unavyoendelea, kwa kuwa sisi ni mataifa mawili na tuna matatizo yanaoingiliana," amesema kupitia hotuba yake kupitia kituo cha radio cha taifa.

Rais Samia, kwa upande wake alisema tu kwamba amekwenda Msumbiji kuthibitisha upya mshikamano baina yao. Amesema "Tanzania iko hapa kuonyesha ushirikiano na Msumbiji katika masuala ya kimaendeleo, amani na usalama."

Hata hivyo viongozi hao wawili hawakuzungumzia kwa kina kuhusu kiini cha mazungumzo yao, lakini Nyusi aliashiria kwamba alikuwa anataka ushirikiano zaidi wa kikanda.

Soma Zaidi:Wakuu wa SADC walaani uasi nchini Msumbiji

Vikosi vya Msumbuji, Rwanda vyakomboa mji muhimu

Kampuni ya Total ya Ufaransa, ina uwekezaji wa kiasi cha dola bilioni 20 kwenye mkoa huo wa Cabo Delgado, unaotajwa kuwa mkubwa zaidi wa nje barani Afrika.

Mashirika: AFPE