1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Ligi ya TFF yaendelea kurindima

Saumu Njama Mhindi Joseph
8 Aprili 2024

Hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itaendelea Kurindima Jumanne (9.4.2024) Simba ikikwaana na Mashujaa katika uwanja wa Tanganyika.

https://p.dw.com/p/4eYR9
Simba vs Al Ahly
Wachezaji wa Simba katika mechi dhidi ya Al Ahly Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Kueleka mchezo huo Kocha Mkuu wa Mashujaa FC Abdallah Bares anasema "mazoezi yameenda vizuri tulichoandaa tumekiandaa na tunaendelea kukiandaa kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho tunaifahamu simba inakuja kucheza na sisi timu nzuri timu imetoka kwenye mashindano lakini kwa upande wetu tutakabiliana nao vizuri tuone na sisi tunaibuka na ushindi katika mchezo huo."

Afisa habari wa simba ahmed Ally "ukifungwa moja umetoka ngoma ikiwa ngumu unatoka na itakuwa kero zaidi kuona mnyama anapoteza mechi dhidi ya mashujaa anaondolewa kwenye mashindano inakuwa ni vurungu kubwa ambayo haina mfano wake kwa maana ya kufanya kazi kubwa wanasimba kuipeleka simba yetu hatua inayofuata na hii mechi siyo nyepesi hata kidogo mashujaa tunawafahamu wanapokuwa nyumbani kwao."

Yanga imejiandaaje?

Young Africans
Wachezaji wa Yanga katika mechi dhidi ya USM Alger ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa Dar Es Salam - Tanzania.Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Na  Jijini Dodoma maandalizi yameendelea kushika kasi kuelekea mechi ya Dodoma jiji ambao wataawalika Yanga katika uwanja wa Jamhuri.

Mwalimu Francis Baraza kocha mkuu wa kikosi cha Dodoma jiji FC kuelekea mechi hiyo ambayo itachezwa jumatano ya april 10  "Tunajua mechi ya FA ni mechi nzuri katika raundi ya 16 sisi tunasema kuwa tupo tayari na najua nacheza na timu bora ambao ni mabingwa katika nchi mimi nitasema maandalizi ni mazuri jaribu kuangalia vijana wapo tayari na tunajua tunacheza na timu nzuri." Alisema Mwalimu Francis Baraza kocha mkuu wa kikosi cha Dodoma jiji FC.

Azam FC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar. Azam FC inakuwa timu ya sita kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo baada ya Singida Black Stars, zamani Ihefu SC, Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.