1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika wa Madagascar asema nchi imo kwenye mkwamo

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Spika wa bunge la Madagascar, Christine Razanamahasoa, amesema nchi hiyo iko katika mkwamo, chini ya kipindi cha mwezi mmoja kabla kufanyika uchaguzi wa rais na wagombea wa upinzani wakiandamana karibu kila siku.

https://p.dw.com/p/4XfmD
Andry Rajoelina Präsident Madagaskar
Rais anayewania kusalia madarakani kwa muhula wa pili nchini Madagascar, Andry Rojaelina (kulia).Picha: picture-alliance/ dpa

Razanamahasoa amewaambia wabunge wa upinzani kwamba Madagascar iko katika hali mbaya, watu wanateseka na wabunge ndio waliosababisha hali hiyo.

Spika huyo ameahidi kufanya kila analoweza kutafuta njia ya kuutanzua mgogoro uliopo kwa maslahi ya taifa.

Mzozo wa kisiasa wanukia Madagascar

Wabunge walimshangilia huku wale walio karibu na rais Andrey Rajoelina pia wakihimiza maridhiano.

Hapo jana wabunge wa upinzani walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumtaka Waziri Mkuu Christan Ntsay ajiuzulu.

Soma zaidi: EU, Marekani zashitushwa na uvunjaji wa haki Madagascar

Ntsay, mshirika wa Rajoelina ni mkuu wa serikali mpaka mkuu mpya wa dola atakapochaguliwa.

Nafasi hiyo kimsingi inatakiwa kushikiliwa na rais wa baraza la seneti ambaye alikataa kwa sababu za kibinafsi.