1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal: Rais Sall asema ataachia madaraka muda wake ukifika

John Juma
23 Februari 2024

Rais wa Senegal Macky Sall amesema ataachia madaraka ifikapo April 2 wakati ambapo muda wake utakuwa unamalizika. Hata hivyo kiongozi huyo hakutangaza tarehe ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4cmzP
Rais wa Senegal Macky Sall.
Rais wa Senegal Macky Sall.Picha: RTS/Reuters

Sall anakabiliwa na shinikizo la kupanga tarehe ya kupiga kura baada ya kuucheleweshw uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Februari 25 hali iliyosababisha mgogoro wa wiki kadhaa.

Huku kukiwa na mvutano wa kijamii na kisiasa, Rais wa Senegal amesema hatotangaza tarehe mpya ya uchaguzi mpaka baada ya mazungumzo ya kisiasa yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo ambapo Sall atafanya majadiliano Jumatatu na Jumanne na wagombeaji urais na wahusika wengine wa kisiasa na kijamii nchini humo.

Katika hatua inayoonekana ya kutuliza maoni ya umma, rais Sall amesema anafikiria kuwaachilia huru viongozi wa upinzani Ousmane Sonko na Bassirou Diomaye Faye walio kizuizini.