1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Scholz aahidi uchunguzi wa haraka kuhusu udukuzi wa Urusi

Iddi Ssessanga
2 Machi 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz siku ya Jumamosi ameahidi ufafanuzi wa haraka, baada ya Urusi kuchapisha rekodi za sauti za maafisa wa kikosi cha anga cha Ujerumani wakijadili msaada wa makombora kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4d6dS
Vatikan | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na PApa Francis
Kansela Olaf Scholz amezungumzia udukuzi wa Urusi akiwa katika ziara mjini Vatikani siku ya Jumamosi, Machi 2, 2024.Picha: Vatican Media/REUTERS

Mazungumzo hayo kati ya maafisa wa ulinzi wa Ujerumani yalichapishwa Ijumaa na mkuu wa shirika la utangazaji la Urusi, RT, Margarita Simonyan.  Akizungumza wakati wa ziara yake Vatikani, Scholz ameitaja kadhia hiyo kuwa "suala zito sana."

Ndani yake, maafisa wandamizi wa jeshi la anga wanajadili uwezekano wa kinadharia wa kupeleka makombora ya Ujerumani aina ya Taurus nchini Ukraine.

Scholz alikataa mara kwa mara kupeleka makombora hayo, licha ya maombi ya mara kwa mara ya Ukraine, akisema anahofia kuitumbukiza Ujerumani zaidi katika vita vilivyoanzishwa na Urusi Februari 2022.

Sauti hiyo pia inahusisha mazungumzo nyeti ya kidiplomasia kuhusu Uingereza kuwa na watu wachache ndani ya Ukraine, kuhusiana na upelekaji wa makombora yake ya Storm Shadow nchini humo. Utajo wa Uingereza unafuatia hasira nchini humo kuhusu kile ambacho London ilikiona kama uzembe wa hapo awali wa Scholz.

Soma pia:Bundestag yapiga kura ya kupinga kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu 

Scholz alikuwa amesema, katika muktadha wa mjadala wa Taurus, kwamba "kile Waingereza na Wafaransa wanachofanya katika suala la udhibiti wa shabaha na kuandamana na udhibiti wa shabaha hakiwezi kufanywa nchini Ujerumani," bila kufafanua zaidi.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Scholz ameutaja udukuzi wa mazungumzo ya Bundeswehr kuwa suala zito sana.Picha: picture alliance/Flashpic

Baadhi waliliona suala hili kama dalili kwamba vikosi vya Ufaransa na Uingereza vinasaidia udhibiti wa makombora ya kasi yaliyotolewa kwa Ukraine. London ilikanusha mara moja jambo hilo kuwa siyo kweli.

Aaliposhinikizwa na mwandishi wa dpa siku ya Jumamosi kuhusu uwezekano wa mzozo wa kidiplomasia kutokana na kudukuliwa kwa mazungumzo ya maafisa wa Bundeswehr, Scholz alisema: "Ndiyo maana hili sasa linafafanuliwa kwa makini sana, kwa kina na haraka sana. Hilo pia ni muhimu."

Mkaguzi wa Jeshi la Anga Ingo Gerhartz alikuwa miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo, ambao inasemekana ulikuwa katika maandalizi ya kumpa taarifa Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius.

Hoja kuhusu muda wa uvujishaji wa sauti hizo

Mazungumzo yaliosikika katika rekodi hiyo yanashughulikia suala la iwapo makombora ya Taurus yana uwezo wa kiufundi wa kuharibu daraja lililojengwa na Urusi hadi Rasi ya Ukrain ya Crimea, iliyochukuliwa na Moscow kinyume na sheria ya kimataifa.

Majadiliano hayo pia yanazungumzia iwapoUkraine inaweza kufanya shambulio hilo bila kushirikisha vikosi vya kijeshi vya Ujerumani. Inabainishwa wazi katika rekodi hiyo kwamba wabunge wa Ujerumani hawako tayari kuipatia Kiev makombora yamasafa marefu.

Vyanzo vya habari viliiambia dpa mapema Jumamosi kwamba rekodi hiyo ni ya kweli na kwamba majadiliano yaliandaliwa kwenye Webex, jukwaa la mikutano la mtandaoni lililoundwa na Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani Pistorius atembelea kambi ya anga ya Holzdorf
Inspekta Jenerali wa kikosi cha Anga cha Bundeswehr Ingo Gerhartz akimkaribisha waziri wa ulinzi Boris Pistorius katika kambi ya wana Anga ya olzdorf. Gerhartz ni mmoja wa waliozungumza kwenye sauti zilizovujishwa na Urusi.Picha: Klaus-Dietmar Gabbert/dpa/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani ilikuwa ikichunguza iwapo mawasiliano hayo yalinaswa. "Ofisi ya Shirikisho ya Huduma ya Kukabiliana na Upelelezi wa Kijeshi imeanzisha hatua zote muhimu," msemaji wa wizara alisema Ijumaa jioni.

Soma pia: Kansela Olaf Scholz akataa kutoa makombora ya Taurus kwa Ukraine

Wabunge wa Kamati ya Usalama wa Ujerumani walijibu kwa wito wa kufanya maboresho. "Tunahitaji haraka kuongeza usalama wetu na ujasusi, kwa sababu ni wazi kuwa tuko hatarini katika eneo hili," Marie-Agnes Strack-Zimmermann, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Bundestag, aliliambia shirika la habari la Redaktionsnetzwerk Deutschland (RND).

"Swali linaloibuka ni iwapo hili ni tukio la mara moja au tatizo la kiusalama," alisema Konstantin von Notz, mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti ya Bunge.

Soma pia:Ukraine yasema ina uhakika Ujerumani itaipatia makombora ya Taurus

Chapisho hilo liliibua uvumi ulioenea juu ya wakati wake, Aliiambia RND kwamba ujasusi ni "sehemu ya sanduku la zana la Urusi la vita mseto," na kuongeza kuwa haishangazi kwamba mazungumzo yalinaswa. "Ilikuwa ni suala la muda kabla ya kuwa hadharani," alisema.

Wengine walikisia kwamba uvujishaji huo wa mazungumzo ya Bundeswehr unaweza kuwa jaribio la Urusi kugeuza mjadala wa umma kutoka kwenye ufichuzi wa hivi karibuni au mazishi ya mpinzani Alexei Navalny.

Ujerumani: Hatutaiacha Ukraine kwenye vita peke yake