1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kongo Felix Tshisekedi kuapishwa kwa muhula wa pili

20 Januari 2024

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anatarajiwa kuapishwa leo kwa muhula wa pili madarakani baada ya kushinda uchaguzi ambao upinzani umesema uligubikwa na visa na udanganyifu na hivyo matokeo yake sio halali.

https://p.dw.com/p/4bUgT
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: AFP

Hafla ya kuapishwa kwa rais huyo mwenye umri wa miaka 60 anayejulikana kwa jina la utani kama "Fatshi" itafanyika katika uwanja wa michezo wa Martyrs wenye uwezo wa kubeba watu 80,000.

Kulingana na mamlaka ya Kongo, marais 18 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Kuapishwa kwake kwa mara ya kwanza kulifanyika mnamo Januari 2019 katika bustani ya Ikulu ya Taifa, baada ya ushindi wa utata dhidi ya Martin Fayulu. Bustani hiyo imekuwa ikitumika kuandaa hafla mbalimbali za serikali.

Mnamo Disemba 20, Wakongomani walipiga kura kumchagua rais, wabunge, magavana wa mikoa pamoja na madiwani.