1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Qatar yashinikiza muafaka Gaza kabla ya Ramadhani

27 Februari 2024

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari, amesema nchi hiyo ina matumaini ya kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hamas kabla ya Ramadhani

https://p.dw.com/p/4cxVb
Ukanda wa Gaza| Mashambulizi ya Israel
Gaza imekabiliwa na mashambulizi mfululizo kwa zaidi ya miezi minne kutoka kwa Israel.Picha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari, amesema nchi hiyo ina matumaini ya kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hamas na inaendelea na juhudi za makubaliano hayo kufikiwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza tarehe 11 mwezi Machi.

Majed al-Ansari, amesema hali katika uwanja wa mapambano bado ni ngumu, lakini wana matumaini huenda makubaliano yakafikiwa hivi karibuni.

Soma pia: Hizbullah yakabliana na Israel kijeshi

Ansari ameyasema hayo baada ya rais wa Marekani Joe Biden, kutangaza kuwa makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa mjini Gaza huenda yakafikiwa siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas vilivyoanza Oktoba 7 hadi sasa vimesababisha mauaji ya zaidi ya Wapalestina 29,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.