1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin:Mataifa ya Magharibi yanawajibika kwa mfumuko wa bei

23 Novemba 2023

Rais Vladmir Putin wa Urusi amekataa ukosoaji wa vita vyake dhidi ya Ukraine wakati pia akiwalaumu viongozi wa magharibi kwa kupanda kwa mfumko wa bei duniani. Kwa mujibu wa Ikulu ya Kremlin,

https://p.dw.com/p/4ZLAD

Putin ameuambia mkutano wa kilele wa nchi tajiri duniani za G20 kwa njia ya video kuwa Urusi haijawahi kuyafuta mazungumzo ya amani na Ukraine. Putin kwa mara nyingine aliyataja mabadiliko ya mamlaka kufuatia maandamano ya kuunga mkono Ukraine kuegemea sera za Ulaya mjini Kyiv katika mwaka wa 2014, ambayo aliyaita mapinduzi ya umwagaji damu, kuwa sababu iliyochochea mzozo kati ya Urusi na Ukraine. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema mkutano huo, ambao aliuhudhuria pamoja na mwenzake wa Italia Giorgia Meloni wakati wa ziara yake mjini Berlin, ulikuwa fursa nzuri kuweka wazi kuwa amani inaweza kurejeshwa kwa urahisi Ukraine kama Urusi itawaondoa wanajeshi wake nchini humo.