1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya washutumiwa kuwaua waandamanaji 12

Grace Kabogo
31 Mei 2023

Mashirika mawili ya kutetea haki za binaadamu yamesema kuwa polisi wa Kenya walihusika katika mauaji ya watu 12, wakiwemo watoto wawili wakati wa maandamano ya upinzani mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/4S1Ry
Waandamanaji walipokuwa wakipambana na polisi wakati wa maandamano Machi 27, 2023 katika eneo la Mathare, Nairobi.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga aliitisha maandamano yaliyolenga kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomuingiza madarakani rais William Ruto pamoja na kupanda kwa gharama za maisha.Picha: TONY KARUMBA/AFP

Taarifa ya mashirika ya Human Rights Watch na Amnesty International iliyotolewa leo, imeeleza kuwa yamerekodi idadi hiyo ya vifo wakati wa siku tatu za maandamano ya kuipinga serikali yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. Kwa mujibu wa mashariki hayo, wakati baadhi ya wahanga walihusika katika maandamano, wengi wa hao 12 walikuwa wapita njia au waliokuwepo kwenye nyumba zao na maeneo ya biashara. Watoto wawili, akiwemo wa miezi minne, pia walikufa kutokana na matatizo ya kiafya baada ya polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi kwenye makaazi ya Kibera. Twakimu za serikali zinaonesha kuwa watu watatu walikufa katika maandamano hayo, akiwemo askari polisi.