1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

OCHA: Watu milioni 3 wameyakimbia makaazi Sudan

8 Agosti 2023

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu OCHA imesema watu wapatao milioni 3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan tangu katikati ya mwezi April.

https://p.dw.com/p/4UtjU
Sudan Darfur
Raia wa Sudan waliokimbia vita katika mkoa wa DarfurPicha: ZOHRA BENSEMRA/REUTERS

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu OCHA imesema watu wapatao milioni 3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan tangu katikati ya mwezi April. Shirika hilo limeeleza kwamba watu wengine zaidi ya 880,000 wamelazimika kukimbia na kwenda nje ya nchi na kwamba wakimbizi wengi wa Sudan wamekwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini.

Shirika hilo la Umoja wa mataifa limesema jumla ya watu milioni 20.3, sawa na asilimia 42 ya wakazi wa Sudan, wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Soma siku 100 za mapigano: Sudan yatimiza siku 100 za mapigano

OCHA pia imesema hali katika eneo la magharibi la Darfur inatia wasiwasi.Jeshi la Sudan linaongozwa na Kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah Burhan limekuwa katika mzozo wa kugombea madarakakati yake na Wanajeshi wa kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na makamu wake wa zamani Mohammed Hamdan Daglona tangu Aprili 15.