1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege za kutafuta wahamiaji zazuiwa kutumia viwanja Italia

8 Mei 2024

Italia imetangaza marufuku kwa mashirika ya hisani kutumia viwanja vya ndege kwenye visiwa vitatu kurusha ndege ambazo husaidia kutafuta boti za wahamiaji wanaohitaji msaada baharini.

https://p.dw.com/p/4fblm
Boti ya Wahamiaji
Ndege za mashirika ya hisani huwasaidia wahamiaji waliokwama bahari ya Mediterrania. Picha: Giacomo Zorzi/ Sea-Watch/REUTERS

Uamuzi huo uliotolewa jana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Italia, unahusu viwanja vya ndege vya visiwa vya Sicily, Pantelleria na Lampedusa ambavyo vipo karibu na njia kuu inayotumiwa na wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.

Tangazo hilo linamaanisha itakuwa vigumu kwa mashirika ya hisani kutumia ndege ndogo kuzunguka baharini kutafuta boti za wahamiaji walio na dharura.

Moja ya mashirika ya hisani la Sea Watch limeutaja uamuzi huo kuwa kitendo cha "kioga" kilichofanywa na maslahi ya kisiasa.

Ndege za mashirika yasiyo ya kiserikali zimekuwa msaada mkubwa kwa wahamiaji wanaokwama baharini na mara zote zimewasaidia waokoaji kuwafikia wale waliokwama.

Hata hivyo operesheni za aina hiyo zinakabiliwa na upinzani mkali tangu serikali ya mrengo mkali wa kulia ya Waziri Mkuu Giorgia Meloni ilipoingia madarakani mwaka 2022.