1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kufanya luteka kubwa ya angani nchini Ujerumani

9 Juni 2023

Jumuiya ya Kujihami ya NATO itafanya mazoezi makubwa kabisa ya kijeshi ya angani kuwahi kufanywa nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4SOS3
 NATO-Manöver | Air Defender 23
Picha: Philipp Hiemer/Bundeswehr

Maafisa wa Marekani na Ujerumani wamesema luteka hizo bila shaka zitakuwa za kuvutia zaidi na zitaonesha kwamba mipaka ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO ni mstari mwekundu kisiasa kwa yeyote atakayejaribu kuuvuka. 

Luteka hizo zimeundwa katika mfumo wa kuiga jibu la shambulizi lolote dhidi ya nchi mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO.

Mnamo Jumatano, maafisa walisema Ujerumani ndiyo itakuwa mwenyeji wa luteka hizo za angani, ambazo zimetajwa kuwa kubwa kabisa kuwahi kufanyika Ulaya katika historia ya muungano huo wa kijeshi.

Urusi yaanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika ukanda wa Arctic

Luteka hizo ambazo zimepewa jina Ulinzi wa Angani 2023 zimepangwa kuanza Jumatatu na zitawashirikisha wanajeshi 10,000, na ndege 250 kutoka nchi 25.

Marekani ambayo ni miongoni mwa waandaaji wakuu wa luteka hiyo, itatuma ndege 100 na wanajeshi 2,000 kushiriki.

Luteni Jenerali wa jeshi la angani la Ujerumani Ingo Gerhartz, amesema wanataka kuonesha kwamba mipaka ya nchi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO ni mstari mwekundu ambao wako tayari kulinda kila sentimita yake.

China yahitimisha luteka ya kijeshi

Lakini kamanda mwengine wa ngazi ya juu wa Ujerumani amesisitiza kuwa luteka hiyo imeandaliwa kwa mfumo wa ‘ulinzi' kuelekea Urusi. Kwa hivyo, ametoa mfano kwamba hawatarusha ndege yoyote kuelekea Kaliningrad, hali inayodhihirisha lengo ni kujihami.

Balozi wa Marekani nchini Ujerumani Amy Gutmann amesema mazoezi hayo yatajumuisha maonyesho ya "kuvutia" ya nguvu kuelekea nchi nyingine duniani.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa Habari katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.

Marekani inatarajiwa kupeleka wanajeshi 2,000 na ndege za vita 100 kwenye mazoezi hayo.
Marekani inatarajiwa kupeleka wanajeshi 2,000 na ndege za vita 100 kwenye mazoezi hayo.Picha: Jane Schmidt/Bundeswehr

Ameendelea kueleza kwamba maonesho hayo yatadhihirisha bila shaka yoyote uwepesi na haraka ya kikosi chao cha washirika katika NATO kama mtoa jibu wa kwanza wakati wa shambulizi.

"Nitashangazwa sana ikiwa kiongozi yeyote duniani akiwemo rais wa Urusi Vladimir Putin, hatatilia maanani kile luteka hizo zitamaanisha kwa msingi wa umoja. Zinamaanisha nguvu ya muungano”.

Marekani na Korea Kusini kufanya luteka ya kijeshi ya siku 10

Mnamo Jumatano, Gerhartz aliwaambia waandishi wa Habari kwamba mazoezi hayo yatavuruga usafiri wa ndege za angani lakini kwa kiasi kidogo tu.

Michael Loh, mkurugenzi wa kikosi cha Walinzi wa Kitaifa wa Marekani, aliunga mkono maoni hayo, akisema kwamba usumbufu unatarajiwa kuwa mdogo.

Lakini chama cha wadhibiti wa trafiki wa anga ya Ujerumani GdF, kimesema mazoezi hayo yanaweza kuwa na "athari kubwa."

Mwenyekiti wa chama hicho Mathias Maas ameliambia shirika la Habari la Ujerumani DPA kwamba mazoezi ya kijeshi ya ulinzi wa angani bila shaka yataathiri pakubwa mpangilio wa safari za ndege.

Maas alitaja takwimu za shirika la kudhibiti trafiki ya anga la Eurocontrol, ambalo lilikadiria kuwa kila hatua moja ya luteka inaweza kusababisha uchelewefu wa hadi dakika 50,000 kwa siku.

Mwandishi: Frank Hofmann

Tafsiri: John Juma