1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwili wa Navalny wabainika kuwa katika hospitali ya Siberia

18 Februari 2024

Jarida moja huru nchini Urusi, Navoya Gazeta limeandika kwamba mwili wa mkosoaji wa Vladimir Putin, Alexei Navalny umehifadhiwa katika hospitali iliyo katika mji wa Salekhard ulio kaskazini wa Siberia.

https://p.dw.com/p/4cYE5
Urusi, St. Petersburg | Maombolezo ya Alexei Navalny
Picha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny, maua na mishumaa vikiwekwa chini wakati watu wakikusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa Alexei Navalny huko St. Petersbiurg, Urusi Ijumaa, Februari 16, 2024.Picha: Dmitri Lovetsky/AP/picture alliance

Taarifa ya gazeti hilo lilonaipinga serikali ya Urusi ambalo kwa sasa linachapishwa kutoka nchini Latvia, imeongeza kusema, kuwa hadi kufikia jana Jumamosi mwili wa mpinzani huyo ulikuwa bado haujafanyiwa uchunguzi. Kifo cha Navalny ambacho hakikutarajiwa na wengi akiwa na umri wa miaka 47, na ambacho kimeripotiwa siku mbilizilizopita kimezusha gadhabu kwa jumuiya ya kimataifa. Novaya Gazeta liliongeza kuwa mtoa taarifa wake wa siri amesema mwili wake ulikuwa umewekewa alama za bluu. Ndugu wa Navalny hadi sasa bado hajapewa nafasi ya kuona mwili wake.