1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtaalamu wa mitandao wa Marekani afungwa jela miaka 21

Tatu Karema
30 Aprili 2024

Mtaalamu mmoja wa mitandao ambaye alifanya kazi kwa muda mfupi katika Shirika la Usalama la Taifa la Marekani (NSA) amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 21 jela kwa kujaribu kuifanyia ujasusi Urusi.

https://p.dw.com/p/4fLIU
Mwanasheria mkuu wa Marekani, Merrick Garland.
Mwanasheria mkuu wa Marekani, Merrick Garland.Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Jareh Sebastian Dalke, mwenye umri wa miaka 32, alifanya kazi chini ya mwezi mmoja katika shirika la NSA, kabla ya kuacha kazi ghafla akitaja matatizo ya kifamilia mwishoni mwa mwezi Juni 2022.

Kulingana na nyaraka za mahakama, katika wiki hizo chache kwenye NSA, Dalke alichapisha hati za siri kubwa na baada ya kuacha kazi, aliziuza kwa dola 85,000 kwa mtu aliyeamini kuwa wakala wa Urusi.

Katika taarifa yake, Mwanasheria Mkuu Merrick Garland alisema kuwa Dalke, ambaye alikuwa amekula kiapo cha kuilinda nchi hiyo, alikuwa anaamini anauza taarifa hizo za siri za usalama wa taifa kwa wakala wa Urusi, ilhali alikuwa anajiingiza katika mtego wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).