1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na China wajadili namna ya kuhitimisha mivutano

Lilian Mtono
10 Novemba 2023

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ameanza mazungumzo na Makamu Waziri Mkuu wa China He Lifeng kabla ya mkutano muhimu wa kilele wa wakuu wa mataifa ya Asia-Pasifiki, APEC.

https://p.dw.com/p/4Ye0R
Waziri wa Fedha wa Marekani ni miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu wa Marekani anayeshiriki juhudi za taifa hilo zua kurejesha uhusiano wa kawaida baina yao
Waziri wa Fedha wa Marekani ni miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu wa Marekani anayeshiriki juhudi za taifa hilo zua kurejesha uhusiano wa kawaida baina yaoPicha: AMIT DAVE/REUTERS

Mkutano huo wa kilele wa APEC unalenga kuhitimisha mivutano licha ya wasiwasi unaoongezeka wa kiusalama.

Mazungumzo hayo ya siku mbili yameanza Alhamisi hii mjini San Francisco ambako mkutano huo wa kilele wa APEC unatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.

Yellen na Lifeng, walijadiliana juu ya wasiwasi kuhusu usawa wa biashara, ushirikiano katika suala la mabadiliko ya hali ya hewa na madeni, miongoni mwa mengineyo.

Yellen aidha amesema kabla ya mazungumzo hayo kwamba Marekani itaendelea kuchukua hatua muhimu za kulinda usalama wao na wa washirika wao na kuahidi kujadiliana kwanza juu ya hatua hizo ili kuzuia migongano.