1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawaorodhesha wa Houthi kama kundi la kigaidi

19 Januari 2024

Jeshi la Marekani limesema limeyalenga makombora 14 yaliyokuwa tayari kurushwa nchini Yemen, baada ya Washington kuwaorodhesha tena wanamgambo wa Houthi kama kundi la kigaidi

https://p.dw.com/p/4bPaF
Yemen | Houthi
Waasi wa Houthi waorodheshwa kama kundi la kigaidiPicha: Osamah Yahya/ZUMA Wire/IMAGO

Katika taarifa, Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani imethibitisha kushambuliwa kwa makombora hayo ya Wahouthi.

Marekani yaharibu makombora 14 ya waasi wa Kihouthi

Wanamgambo hao ambao tayari wamekabiliwa na mashambulizi kadhaa ya makombora ya angani, wameilenga meli moja ya mizigo ya Marekani kufuatia tangazo hilo la Marekani la kuwaorodhesha kama kundi la kigaidi.

Wanamgambo hao wameapa kuendelea na mashambulizi hayo ambayo wanasema ni ya kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.