1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marafiki kupostiana mtandaoni siku ya "Birthday"

14 Mei 2024

Siku hizi ni lazima kwanza uanzie kuweka picha mtandaoni ambako huko ndugu na jamaa nao watakuandikia jumbe zao za kheri. Lakini vipi ikitokea marafiki zako hawajafanya hivyo?. Wapo ambao urafiki wao unafifia kama asipomposti rafikye mtandaoni kwenye siku yake ya kuzaliwa. Wewe vipi unaona ni sawa ?.

https://p.dw.com/p/4fq7C

Karibu kwenye kipindi cha Vijana Mchamchaka, Miaka ya hivi karibuni utamaduni wa kutakiana kheri ya kuzaliwa umebadilika hasa baada ya kuwepo kwa ongezeko la watumiaji wa mitandao ya kijamii na majukwaa ya Kidijitali.

Vijana ambao ndio watumaiji wakubwa wa mitandao na majukwaa hayo sasa wameyageuza kuwa kama eneo la kutakiana kheri ya siku ya kuzaliwa. Baadhi huenda mbali zaidi na kupiga picha maalumu kwaajili ya siku ya kuzaliwa na kuwatumia jamaa na rafiki zao ili wazipakie mitandaoni na kuambatanisha ujumbe wa kuwatakia Kheri. 

Mitandao hiyo hiyo sasa imegeuka kuwa sehemu ya kupimana urafiki, undugu na kwamba mtu asipokutakia heri ya kuzaliwa kwa kupakia picha yako kwenye mitandao ya kijamii au majukwaa ya kidijitali basi unaamini kwamba haumjali au urafiki wenu una walakini..  Vijana mchaka mchaka inawauliza kuhusu haya yanayoendelea.

Je, wewe una maoni gani juu ya hili?.