1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

City kuchuana na Inter katika fainali ya Ligi ya Mabingwa

10 Juni 2023

Manchester City itateremka dimbani Ataturk Olympic mjini Istanbul kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza na kushinda mataji matatu msimu huu watakapocheza dhidi ya Inter Milan katika mechi ya fainali.

https://p.dw.com/p/4SPaA
Fußball Pokal UEFA Champions League
Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Champions LeaguePicha: FrankHoermann/SVEN SIMON/picture alliance

Vijana wa Pep Guardiola tayari wameshinda taji la Ligi Kuu ya Premia na Kombe la FA.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu kwa Manchester City kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, na walifungwa na Chelsea msimu wa mwaka 2020-21.

Guardiola anasaka taji lake la Ulaya kwa mara ya kwanza tangu alipofanya hivyo mnamo mwaka 2011 akiwa mkufunzi wa Barcelona, ambapo pia alishinda mataji matatu miaka miwili kabla ya hapo.

Fußball Champions League | Inter Mailand vs AC Mailand
Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez akisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya AC Milan.Picha: Mike Hewitt/Getty Images

Manchester United ndio klabu pekee ya Uingereza iliyowahi kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja. Mnamo msimu wa mwaka 1998-99, Mashetani hao wekundu walishinda taji la Ligi Kuu ya Premia, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Inter Milan haijapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi ya leo, japo ina historia nzuri ya Ulaya tofauti na City, kwani wamewahi kushinda Ligi ya mabingwa barani Ulaya mara tatu.

Mara ya mwisho kushinda taji hilo ilikuwa mnamo mwaka 2010, wakati huo ikitiwa makali na Jose Mourinho.