1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man U yatupwa nje michuano ya Champions League

John Juma
13 Desemba 2023

Manchester United ya Uingereza imetupwa nje ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na vilevile haitashiriki Ligi ya Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kundi lao kufuatia kushindwa kwao 1-0 na Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/4a6J4
Manchester United ilipokutana na Bayern Munich.
Manchester United ilipokutana na Bayern Munich kwenye mchezo wa Champions League mnamo Disemba 12, 2023.Picha: Martin Rickett/PA Images/IMAGO

Union Berlin ya Ujerumani pia imeachwa mikono mitupu baada ya kushindwa mabao 3-2 na miamba wa Uhispania, Real Madrid.

Copenhagen iliambulia nafasi ya pili na kufuzu hatua ya mtoano ya 16 bora kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Galatasaray, ambao wamefuzu Ligi ya Ulaya.

Napoli ilipiga hatua mbele baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Braga ya Ureno.

Timu zinazomaliza katika nafasi ya kwanza na pili zinafuzu moja kwa moja katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa, huku timu ya tatu ikielekea kucheza Ligi ya Ulaya na inayomaliza nafasi ya nne inatupwa nje ya mashindano hayo mawili.