1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Makumi ya wahamiaji wanusurika wakivuka kuingia Uingereza

15 Desemba 2023

Mamlaka ya baharini ya Ufaransa imewaokoa wahamiaji 66 waliokuwa wakijaribu kuvuka ujia wa maji wa Uingereza usiku wa kuamkia leo, japo mmoja kati yao alipoteza maisha.

https://p.dw.com/p/4aBik
Ujia wa maji baina ya Ufaransa na Uingereza
Ujia wa maji baina ya Ufaransa na Uingereza Picha: Gareth Fuller/PA Wire/dpa/picture alliance

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa, mtu mwingine aliokolewa akiwa katika hali mbaya na amesafirishwa kwa helikopta hadi hospitali katika bandari ya Ufaransa ya Calais.

Mtu aliyepoteza maisha alikuwa amepoteza fahamu wakati alipochukuliwa na kwamba hawakufanikiwa kumuokoa.

Inaripotiwa kuwa, boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji hao ilikuwa imeharibika kidogo na kwamba baadhi ya wahamiaji walitumbukia baharini.