1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Makabiliano baina ya majeshi hasimu yapamba moto Sudan

Bruce Amani
6 Juni 2023

Makundi ya kijeshi yanayopigana nchini Sudan yamepambana leo kupitia mashambulizi ya angani ya ardhini, wakati machafuko yanayoongezeka na vitendo vya kutokutii sheria vikisambaa.

https://p.dw.com/p/4SGcY
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: AFP

Makundi ya kijeshi yanayopigana nchini Sudan yamepambana leo kupitia mashambulizi ya angani ya ardhini, wakati machafuko yanayoongezeka na vitendo vya kutokutii sheria vikisambaa. Wakaazi wa mji huo wanakabiliwa na uhaba wa chakula na madawa. Makombora na mashambulizi ya kutokea angani yaliendelea usiku kucha, huku wakaazi wa kusini na mashariki mwa Khartoum na Bahri kaskazini wakiripoti kusikia milio ya makombora na makabiliano ya bunduki leo asubuhi. Mashirika ya misaada yameshindwa kuendesha operesheni zao katika maeneo yaliyoathirika. Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces - RSF, ambayo sasa yako katika wiki yake ya nane, yamewauwa mamia ya raia, na kusababisha karibu 400,000 kukimbilia nchi jirani na zaidi ya milioni 1.2 kuondoka mji mkuu na miji mingine. Saudi Arabia na Marekani zilisimamia mpango wa kuwekwa chini silaha kwa ajili ya kupelekwa msaada wa kiutu. Hata hivyo mazungumzo yalivunjika wiki iliyopita.