1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Burundi: Maelfu waachwa bila makazi kufuatia mafuriko

13 Aprili 2023

Afisa mmoja nchini Burundi amesema mafuriko yaliyoshuhudiwa wiki nzima katika sehemu moja magharibi mwa nchi hiyo yamepelekea maelfu ya watu kuachwa bila makazi.

https://p.dw.com/p/4PzaG
Burundi Überschwemmung in der Gemeinde Gatumba
Picha: Antéditeste Niragira/DW

Mkuu wa utawala katika wilaya ya Mutimbuzi Simeon Butoyi, amesema, zaidi ya familia elfu 4 zinazoishi katika kijiji cha Gatumba zimeachwa bila makazi huku wengine wakisema wanalala nje huku wakipigwa na baridi kali nyakati za usiku.

Soma pia: Mabadiliko ya tabia nchi yasababisha watu zaidi ya 100,000 kuachwa bila ya makazi

Kiongozi mmoja wa eneo hilo Lucie Gahimbare amesema eneo hilo hukumbwa na hasara sawa na hiyo katika kila msimu wa mvua pale mto Rusizi unapofurika na kuvunja kingo zake. Mto huo ndio unaoitenganisha Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.