1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madagascar yataka balozi wa Umoja wa Ulaya abadilishwe

5 Aprili 2024

Madagascar imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kumbadilisha balozi wake katika taifa hilo la mashariki mwa Afrika ambaye alikosoa sheria ya hivi majuzi inayoruhusu kuhasiwa kwa wabakaji watoto.

https://p.dw.com/p/4eTZW
Rais  Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar.
Rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar.Picha: Lewis Joly/REUTERS

Mapema mwezi Februari, bunge la Madagascar lilipitisha mswada unaoruhusu kuhasiwa kwa kemikali na upasuaji watu wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wadogo.

Balozi wa Umoja wa Ulaya, Isabelle Delattre Burger, aliikosoa sheria hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari na kuitaja kuwa kinyume cha katiba ya Madagascar na kwa kanuni za kimataifa.

Soma zaidi: Kimbunga Gamane chaua watu 11 Madagascar

Sheria hiyo pia iliyokosolewa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, kwa kuitaja sheria hiyo kama "ukatili, unyama na udhalilishaji".

Msemaji wa Tume ya Ulaya, Nabila Massrali, alisema waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo alimwandikia barua kamishna mkuu wa Umoja wa Ulaya kuelezea kutokuridhishwa na kauli ya balozi huyo.

Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa Madagascar, ambayo inategemea sana misaada ya kimataifa na  karibu asilimia 75 ya wakaazi milioni 29 wanaishi katika umaskini.