1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

La Liga; Real Madrid yadondosha poiti mbili

6 Novemba 2023

Real Madrid walishindwa kuendeleza ushindi wao baada ya Clasico na kudondosha pointi mbili katika mbio za kuwania ubingwa wa La Liga kwa sare ya 0-0 dhidi ya Rayo Vallecano jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/4YTFa
Spanien Jude Bellingham
Wachezaji wa Real MadridPicha: Josep Lago/AFP/Getty Images

Sare hiyo inaiweka Madrid katika nafasi ya pili kweye jedwali, pointi mbili nyuma ya vinara Girona, waliotoka nyuma na kuwashinda Osasuna 4-2.  Barcelona baada ya kuangukia ushindi wa bao moja bila dhidi ya Real Sociedad siku ya Jumamosi imetulia katika nfasi ya tatu ikiwa na pointi 27.

Soma pia: Vinicius Jr. abaguliwa tena Uhispania

Athletic Bilbao ilipanda hadi nafasi ya tano kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Villarreal jana Jumapili. Wachezaji ndugu Nico na Inaki Williams waliifungia Bilbao katika kipindi cha kwanza baada ya Inigo Ruiz de Galarreta kufunga bao la kwanza dakika ya pili ya mchezo. Mabao ya Villareal walifungwa haraka haraka dakika ya 86 na 87 mtawalia kupitia wachezaji Gerard Moreno na Alexander Sørloth.

Kwingineko Valencia walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Granada kwa mkwaju wa penalti tata kupitia mchezaji Pepelu, huku Alaves wakiilaza Almeria iliyo mkiani katika jedwali la La Liga bila ya ushindi hata mmoja kwa bao moja bila.