1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kylian Mbappe kipenzi cha PSG tena

28 Agosti 2023

Haikuchukua muda mrefu kwa Kylian Mbappe kupendwa tena na mashabiki wa Paris Saint Germain baada ya ule mzozo uliokuwepo kuhusiana na mkataba wake, jambo lililompelekea kukosa mwanzo wa msimu mpya wa Ligue 1.

https://p.dw.com/p/4VevS
Kandanda Mitchel Bakker
Kylian Mbappe (Kulia) akisherehekea na mchezaji mwenzake Mitchel Bakker (kushoto)Picha: Michel Euler/AP Photo/picture alliance

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbappe kwa mara ya kwanza msimu huu alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha PSG na akafunga mabao mawili walipokuwa wakicheza na Racing Lens na kupata ushindi wa 3-1.

Katika mechi ya pili ya PSG Mbappe pia alikuwa miongoni mwa wafungaji ingawa aliingia kama mchezaji wa akiba.

Vyanzo: Reuters/DPAE