1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Kundi la Hezbollah lashambulia kamandi ya kijeshi ya Israel

Saumu Mwasimba
9 Januari 2024

Hezbollah imefahamisha kwamba imeshambulia katika makao makuu ya jeshi kwenye eneo la Safed ikiwa ni mara ya kwanza kuwahi kulilenga eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4b1DB
Hezbollah yasema yalipiza kisasi kwa kuishambulia Israel
Hezbollah yasema yalipiza kisasi kwa kuishambulia IsraelPicha: AFP

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon,limesema leo kwamba limefanya shambulizi la droni dhidi ya kituo cha kamandi ya jeshi la Israel kama sehemu ya kujibu mauaji ya kiongozi wake mwandamizi Wissam Tawil yaliyofanywa jana Jumatatu na mauaji ya wiki iliyopita ya naibu mkuu wa kundi la Hamas.

Kundi hilo limefahamisha kwamba limeshambulia katika makao makuu ya jeshi kwenye eneo la Safed ikiwa ni mara ya kwanza kuwahi kulilenga eneo hilo.