1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJapan

Kishida: Jiografia ya Noto yakwamisha uokoaji Japan

Josephat Charo
4 Januari 2024

Maelfu ya waokoaji wameendelea na kazi ya kuwatafuta watu walionusurika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea siku ya mwaka mpya lililowaua watu wasiopungua 78.

https://p.dw.com/p/4aquk
Kishida amesema watatumia uwezo wao wote kuwaokoa watu wengi kadri itakavyowezekana
Kishida amesema watatumia uwezo wao wote kuwaokoa watu wengi kadri itakavyowezekana Picha: K. Narax/Future Image/IMAGO

Waokoaji hao wana matumaini ya kuwaokoa manusura wengi kadri itakavyowezekana katika kipindi cha siku tatu muhimu za uokozi kinachokamilika leo mchana.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, amesema kuna watu wengi walionasa katika majengo yaliyoanguka wanaosubiri kuokolewa na jiografia ya eneo la Noto imeifanya kazi ya uokozi na kuwatafuta manusura kuwa ngumu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi habari waziri mkuu Kishida pia amesema watatumia uwezo wao wote kuwaokoa watu wengi kadri itakavyowezekana kufikia jioni majira ya Japan wakati saa 72 zitakapokamilika tangu kutokea kwa janga hilo.

Amesema wamefanya kila linalowezekana kutoa msaada unaohitajika na shughuli za kuyajenga upya maeneo yaliyoathiriwa.