1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aendelea kupata nafuu baada ya upasuaji.

Zainab Aziz
10 Juni 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji. Papa Francis, hatahudhuria sala ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/4SQHf
Papst Franziskus
Picha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Papa Francis anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo na hivyo hatahudhuria sala ya Jumapili. Haya ni kwa mujibu wa daktari wake Sergio Alfieri.

Alfieri, aliyemfanyia upasuaji papa Francis, amewaambia wanahabari kwamba kiongozi huyo wa kanisa katoliki hana homa, na moyo wake pia unafanya kazi vizuri.

Lakini madaktari wamependekezea kutohudhuria sala hizo za Jumapili za umma kuepusha shinikizo katika misuli yake ya tumbo.

Daktari Alfieri amesema kwa kawaida baada ya upasuaji kama huu, mtu hulazwa hospitalini kwa kati ya siku nne na tano.

Alfieri ameongeza kuwa wanatumaini kumshinikiza papa kubaki hospitalini kwa wiki moja zaidi ili kumuwezesha kurejea kufanya kazi kwa nguvu zaidi na usalama lakini akasema uamuzi wa kutoka hospitalini ni wa papa mwenyewe.