1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa ISIS Mashariki mwa Syria, auwawa na Marekani

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema, imemuua kiongozi wa kundi linalojitta Dola la Kiislamu IS la Magharibi mwa Syria, Usamah al-Muhajir, katika shambulio la Julai 7.

https://p.dw.com/p/4TdkE
Ndege ya droni ya MQ-9
Ndege isiyo na rubani ya Marekani chapa MQ-9 huko SyriaPicha: U.S. Air Force/AP/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema, imemuua kiongozi wa kundi linalojitta Dola la Kiislamu IS la Magharibi mwa Syria, Usamah al-Muhajir, katika shambulio la Julai 7.Jeshi la Syria lapokea sifa kwa kumuuwa kiongozi wa IS

Kwenye taarifa yake, Marekani imesema shambulio hilo la Ijumaa lilifanyika kwa kutumia ndege isiyo na rubani chapa MQ-9 wakati al Muhajir alipokuwa akiendesha pikipiki kwenye mkoa wa Aleppo.

Soma pia. Jeshi la Marekani lashambulia nchini Syria na kuua watu 10

Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Marekani imeongeza kuwa ndege ya droni iliyomuuwa kiongozi huyo wa IS, ndiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa uchokozi na ndege ya Urusi kwa takriban saa mbili mapema siku hiyo hiyo ya Ijumaa.

Awali Jumamosi, jeshi la Marekani lilitoa taarifa likidai kuwa ndege za kivita za Urusi zimekuwa zikizichokoza ndege za Marekani zisizo na rubani kwa siku tatu mfululizo ndani ya wiki moja katika anga la Syria.