1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Gamane chasababisha vifo vya watu 18 Madagascar

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Kimbunga Gamane kimesababisha vifo vya watu 18 na wengine wanne hawajulikani walipo, baada ya kupiga upande wa kaskazini mwa Madagascar mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/4eGtK
Kimbunga Freddy |Madagascar
Kimbunga Freddy kilichoipiga Madagascar mwaka 2023Picha: NASA VIA REUTERS

Kimbunga Gamane kimesababisha vifo vya watu 18 na wengine wanne hawajulikani walipo, baada ya kupiga upande wa kaskazini mwa Madagascar mapema wiki hii.

Mamlaka zinasema kwamba kimbunga hicho pia kimesababisha mafuriko makubwa ambayo kwa sehemu yalizamisha vijiji vizima, kusababisha watu kuhama na kuathiri wakaazi wapatao 47,000. Taarifa ya ofisi ya taifa ya kukabiliana na maafa inasema kulitokea maporomoko ya ardhi yaliyojeruhi watu watatu.

Kimbunga Gamane kiliikumba Madagascar mapema siku ya Jumatano lakini sasa kimedhoofika na kuacha uharibifu mkubwa. Katika mikoa ya Diana na Sava iliyoko Kaskazini, madaraja na barabara vilisombwa na maji huku nyumba na mashamba ya mpunga navyo vikizamishwa na mafuriko.Watu 11 wafa kwa kimbunga nchini Madagascar

Wakaazi walionekana wakipiga makasia kuzunguka vijiji vyao kwa mitumbwi ili kuwasaidia wengine waliokwama katika nyumba zao huku kiwango cha maji kikikaribia kufikia paa za baadhi ya majengo.