1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Steinmeier ausifu uongozi wa Stoltenberg

Lilian Mtono
11 Novemba 2023

Rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemsifu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg kwa uongozi wake katika nyakati ngumu.

https://p.dw.com/p/4YgrH
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO jens Stoltenberg akizungumza na waandishi wa habari mjini Morocco katika mkutano wa IMF na Benki ya Dunia, Oktoba 11, 2023
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO jens Stoltenberg akizungumza na waandishi wa habari mjini Morocco katika mkutano wa IMF na Benki ya Dunia, Oktoba 11, 2023Picha: Susana Vera/REUTERS

Rais Frank-Walter Steinmeier amesema hayo katika hafla ya kumtunuku Tuzo ya Henry A. Kissinger, mjini Berlin jana Ijumaa.

Steinmeier amesema Stoltenberg ameiongoza NATO katika kipindi cha misukosuko na kuhakikisha ilikivuka salama, pamoja na kuiandaa jumuiya hiyo kwa mabadiliko makubwa ya sasa na siku zijazo.

Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Norway ameongoza NATO kwa miaka 9, na muda wake wa kuwa madarakani imeongezwa hivi karibuni kutokana na vita vya Ukraine na masuala mengine.

Mwaka jana, Steinmeier alitunukiwa Tuzo hiyo ya kila mwaka inayotolewa na Taasisi ya America Academy ya mjini Berlin, iliyopewa jina la Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Henry A. Kissinger.