1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaishambulia tena Lebanon

Tatu Karema
26 Februari 2024

Duru za usalama nchini Lebanon zinasema Israel imeyashambulia yale inayodai ni maeneo ya kundi la Hizbollah karibu na mji wa Baalbek nchini Lebanon na kuwaua wanachama wawili wa kundi hilo.

https://p.dw.com/p/4cuDi
Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Israel kusini mashariki mwa Lebanon.
Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Israel kusini mashariki mwa Lebanon.Picha: Taher Abu Hamdan/Xinhua/picture alliance

Shambulizi hilo ni la kwanza la aina hiyo mashariki mwa Lebanon tangu kuanza kwa uhasama kati ya Israel na kundi hilo baada ya kuzuka kwa vita katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limesema mashambulizi hayo yalilenga mifumo ya ulinzi ya anga ya Hezbollah kulipiza kisasi dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran kwa kuiangusha droni yake moja kusini mwa Lebanon mapema leo.

Chanzo kimoja cha Hizbullah kimethibitisha idadi hiyo ya vifo.

Chanzo kingine kimesema kuwa mashambulizi ya Israel yalilenga jengo linalotumiwa na Hizbollah katika kitongoji hicho cha Baalbek.

Vyanzo vyote viwili vilizungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kukosa idhini ya kuzungumza na waandishi habari.