1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton dereva bora kabisa katika historia ya F1

16 Novemba 2020

Dereva Lewis Hamilton anaendelea kumwagiwa sifa kutoka kote ulimwenguni baada ya kubeba taji lake la saba la dunia katika mashindano ya mbio za magari ya Formula One. 

https://p.dw.com/p/3lMrO
Formel 1 | Der große Preis der Türkei in Istanbul - Lewis Hamilton
Picha: Tolga Bozoglu/REUTERS

Muingereza huyo wa timu ya Mercedes, amejiunga na Mjerumani Michael Schumacher wa timu ya Ferrari kuwa dereva mwenye mafanikio makubwa kabisa katika historia ya Formula One.

Hamilton mwenye umri wa miaka 35 alionyesha umahiri wake wa uendeshaji katika ushindi wa jana wa mashindano ya Grand Prix nchini Uturuki. Amesema mataji saba ni kitu cha ajabu huku akiwapongeza wote wanaofanya kazi nyuma ya pazia. "Nadhani mwaka huu umekuwa tofauti katika kupigania kitu kikubwa zaidi kuliko taji la saba la ulimwengu. Tunachohitajika kufanya, kitu ambacho hatujakifanya ni kuwa tunahitaji kuja pamoja. Tunapaswa kushinikiza mabadiliko, tunahitaji usawa, katika sekta mbalimbali, tunahitaji kuona, tunahitaji watoto kuona uwakilishi zaidi wa yule unayemfahamu, uwakilishi wao katika sekta mbalimbali"

Na ametuma onyo kwa wapinzani wake: kwamba anahisi ndio mwanzo tu wa kujiimarisha na kuwa bora hata Zaidi na hana mpango wowote wa kuondoka kwa sababu bado hajafikia ukomo.

Afp, ap, reuters, dpa