1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yajisafishia njia 16 bora Champions League

29 Novemba 2023

Klabu ya soka ya Ujerumani, Borussia Dortmund, imejikatia tiketi ya kusonga hatua ya mtoano kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, Champions League, baada ya kuichapa bao 3-1 klabu ya soka ya Italia, AC-Milan.

https://p.dw.com/p/4ZYdU
Champions League
Kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus kwenye moja ya mechi za timu hiyo.Picha: Ralf Ibing/firo Sportphoto/dpa/picture alliance

Mkwaju wa penalti uliowekwa wavuni na kiungo Marco Reus, na magoli mengine mawili yaliyofungwa na wachezaji Jamie Bynoe-Gittens na Karim Adeyemi ndiyo yaliipatia ushindi Dortmund na kufifisha zaidi ndoto za AC Milan kusonga mbele.

Dortmund inaongoza kundi F kwa alama tatu zaidi mbele ya vigogo wa Ufaransa, klabu ya soka ya Paris Saint-Germain, na miamba hiyo miwili itakutana mwezi ujao kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

AC Milan nayo itasubiri miujiza kuona iwapo itamudu kusonga mbele kutegemeana na matokeo yake kwenye mchezo dhidi ya mshika mkia wa kundi F klabu ya Newcastle United.